'Ona’,funzo kwa wasanii

advertise here

 


Wasanii Ay, Madee na mtayarishaji mkongwe  wa muziki nchini Master J kwa pamoja wameitabiria makubwa album ya Marco Chali ‘Ona’ inayotarajia kutoka siku ya ijumaa 28, mei.

 


Kwa upande wake Ay anasema ‘’nimesikiliza project yake, ni nzuri sana ina nyimbo ambazo zina- content, ni nadra kuzisikia, inafanya sikio liweze ku-enjoy muziki kwani linachoka kusikia vitu vya aina moja kwa muda mrefu, hii ni kati ya Album classic kabisa ninayotabiri nyimbo zake kuishi kwa kipindi kirefu sana’’.


Madee pia anasema “watu bado tunaishi kila siku, tumezoea kusikiliza nyimbo leo kesho hazipo, lakini album ya Marco Chali itabakia milele hata kama siku moja yeye asipokuwepo, ajue kuwa itabaki na watu wataisikiliza, Ona itakuwa darasa kwa watu wengine.


Mkurugenzi mtendaji wa MJ Records ambaye pia ni mtayarishaji mkongwe wa muziki Master J, amesema “ili wasanii wetu waweze kufanikiwa katika soko la muziki kimataifa ni vizuri wakatumia muda wao kujifunza kitu kutoka kwenye album hiyo ijayo kwani wataenda kushindana na wale ambao walichukua Grammy, kuna mtu ambaye alichukua Grammy  level ya muziki wake ambao anaufanya ni mkali lakini hauwezi kufikia kwenye hii Ona, hii itumike kama darasa ili tuweze kufika kwenye hizo tuzo za Grammy”.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE