Picha; Dimpoz Afika Macca Kufanya Ibada Takatifu ya Umrah

MBONGO Fleva mwenye uwezo wa juu, Omari Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz leo Mei 9, 2021 kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka kuwa amefanikiwa kusafiri hadi Macca na kufanya ibada takatifu ya Umrah.

ALHAMDULILAH šŸ™šŸ•‹❤️: Mwaka Juzi nilitamani kuwa mahali hapa kwa ajili ya ibada takatifu ya Umrah lakini kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu haikuwezekana nikaishia kulazwa tena kitandani lakini sikufa moyo kwani Mwenyezi Mungu yeye ndiye mpangaji wa kila jambo na anapokupa mitihani basi jua ni kipimo cha imani yako kwake. Sina mengi zaidi ya kujiombea Dua na kuwaombea watu wote Allaah atujaalie kila jema tunalomuomba, atupe afya na uzima,atuondolee dhiki atupe na faraja, atuzidishie ridhiki, atusamehe madhambi yetu, apokee funga zetu, atuzidishie upendo miongoni mwetu Inshaallaah šŸ¤²šŸ¾❤️

Ameandika Ommy Dimpoz.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE