.

5/27/2021

Qatar Kutoa Dola Mil.500 Kuijenga Gaza

QATAR imesema itatoa msaada wa dola milioni 500 ili kuijenga tena Gaza, kufuatia mashambulizi ya anga ya siku 11 yaliyofanywa na Israel dhidi ya Ukanda huo.

 

Taifa la Qatar linatajwa kuwa mshirika mkuwa wakundi la Hamas linalodhibiti Ukanda wa Gaza, shirika la habari la Qatar QNA limesema kwamba fedha hizo zitatumika kuwasainia wakazi wa Gaza kukabiliana na changamoto za maisha zilizosababishwa na mashambulio ya Israel ya hivi karibuni ya Israel.

 

Fedha hiyo zitatumika zaidi katika ujenzi wa vituo vya huduma muhimu pamoja na nyumba ambazo ziliharibiwa. Katika siku 11 za mashambulizi ya anga ya Israel katika eneo la Gaza, Wapalestina 254 wameuawa, ikiwa ni pamoja na watoto 66, na watu wengine 1,900 wamejeruhiwa kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza.

 

Kwa upande wa Isarel, makombora kutoka Gaza yamesaabisha vifo vya watu 12 na kujeruhi wengine wapatao 357.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger