Rais Kagame kuwa wa kwanza kuleta kiwanda chanjo ya corona AfrikaRais wa Rwanda Paul Kagame amesema Taifa lake litakuwa la kwanza kuleta chanjo ya mRNA barani Afrika wakati Afrika ikipambana na janga la virusi vya corona.


“Rwanda inafanya kazi na washirika ili kuwa ya kwanza kutengeneza chanjo ya mRNA barani Afrika,” Kagame katika mkutano wa kwenye mtandao wiki hii katika mkutano ulioitishwa na jopo huru la kukabiliana na janga la corona ingawa hakutoa ufafanuzi.


Waziri wa Afya wa Rwanda, Luteni Kanali Dk.Tharcisse Mpunga ameliambia Shirika la utangazaji la Rwanda kuwa mjadala huo ulikuwa ni wa kuleta kiwanda cha chanjo Rwanda.


“Hii inaweza kuwa hatua kubwa kwa Rwanda na Afrika kupata chanjo…tunategemea kuwa punde mijadala hii itazaa matunda,” Dk. Mpunga amesema Alhamisi usiku.


Aidha, Kagame ameongeza kuwa: “Ikiwa kama Afrika bado inategemea chanjo kutoka mabara mengine, tutakuwa nyuma kwenye foleni mara zote panapokuwa na uhaba,” amesema Kagame kwenye mjadala ulioongozwa na aliyekuwa rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf na Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand Helen Clark siku ya Jumanne.


Mamlaka ya Rwanda haijatoa ufafanuzi ya namna kiwanda hicho kitawekwa Rwanda.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE