Rais Kagame: 'Ninataka kushuhudia haki inatendeka kwenye kesi ya Rusesabagina'

 


Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema anataka kuona haki inatendeka katika kesi ya Paul Rusesabagina, anayeelezwa kuwa shujaa katika filamu ya mwaka 2004 ya Hollywood ya Hotel Rwanda kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Kifaransa, France 24, rais ameonya vitendo vya ''kibaguzi'' dhidi ya mifumo ya kimahakama.


'' Nataka kushuhudia mwenyewe haki katika kesi hiyo. Kwanini unafikiria haki ni ya Ulaya au Marekani au kwa mwingine yeyote lakini sio sisi?


''Ni kama vile jambo pekee kuhusu haki nchini Rwanda au Afrika lazima lisimamiwe na Ulaya au Marekani au sehemu nyinginr. Hapana, hapana kabisa,'' alisema Rais Kagame.


Bw. Rusesabagina anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi yanayohusiana na mashambulizi mabaya nchini Rwanda mwaka 2018 na 2019 yaliyofanywa na FNL, kundi lililo chini ya mwamvuli wa muungani wa MRCD wa vyama vya upinzani ambao yeye ni makamu wa rais.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE