.

5/25/2021

Rais Mwinyi afanya uteuzi wa Mkurugenzi ZBC na Taasisi nyingine

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt. Saleh Y. Mnemo kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Nasriya M. Nassor ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji.
Khamis Siasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti huku Shaib I. Moh’d akimteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana.

Rais Mwinyi pia amemteua Salum Issa Ameir kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana na Hassan K. Hassan ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo.

Aidha, Rais amemteua Ameir Moh’d Makame kuwa Kamishna wa Idara ya Michezo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger