.

5/24/2021

Rais Samia Akutana na Dangote

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Mei 24, amekutana na kufanya mazungumzo na mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote, ambaye amewekeza katika kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa saruji mkoani Mtwara.

Baada ya mazungumzo hayo, Alhaji Dangote amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya biashara nchini na amemuahidi kuwa kampuni yake ambayo imewekeza dola milioni 770 za Kimarekani hapa nchini, itaendelea kuwekeza katika maeneo mengine ikiwemo mpango wake wa kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea.

Amesema, kutokana na kubadilika na kuimarika kwa mazingira ya biashara nchini,  atawahimiza Wafanyabiashara na Wawekezaji wenzake kuwekeza Tanzania kwa kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana nao.

“Tutaendelea kuwekeza Tanzania ili kuzalisha ajira, mapato ya nchi na kuinua ustawi wa Wananchi wa Tanzania, nadhani anahitaji kuungwa mkono katika hili na tumemuahidi kuwa tutaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa hapa Tanzania ili kuunga mkono anachokifanya, sisi tutazalisha ajira,” amesema Alhaji Dangote.

Kwa upande wake, Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Alhaji Dangote kwa uwekezaji alioufanya hapa nchini, na amemhakikishia kuwa Serikali itahakikisha uwekezaji wake na wawekezaji wengine unalindwa kwa manufaa ya pande zote mbili.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger