Rais wa Mali, Waziri Mkuu washikiliwa na jeshi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Maafisa wa kijeshi wa Mali waliokasirishwa na mabadiliko ya baraza la mawaziri wanamshikilia Rais na Waziri Mkuu katika kambi ya jeshi, hatua inayolaaniwa vikali na Jumuiya ya Kimataifa na kutaka waachiliwe huru.

Mali Präsident der Übergangsregierung Bah N'Daw

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza imetoa wito wa kuachiliwa huru mara moja kwa Rais Bah N’Daw na Waziri Mkuu Moctar Ouane, ambao wameshikiliwa katika kambi ya kijeshi.

Kukamatwa kwao viongozi hao wanaongoza serikali ya mpito ambayo iliundwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti, kumeongeza hofu ya kutokea mapinduzi mengine. Viongozi hao walikamatwa baada ya kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri mapema jana ili kutuliza ukosoaji mkubwa uliokuwa ukiikabili serikali yao ya mpito.

Aidha Umoja wa Ulaya umesema uko tayari kuzingatia kuwachukulia hatua viongozi wa kisiasa na kijeshi ambao wanazuia kufanyika mabadiliko nchini Mali.

“Tunalaani kilichotokea Mali katika masaa machache yaliyopita, utekaji nyara wa Rais na Waziri Mkuu, na tunaunga mkono ujumbe uliotumwa na SADC na Umoja wa Afrika,” amesema Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya.

Michel amesema kwa pamoja wanatoa  wito wa kurudishwa kwa serikali ya mpito, na kwamba klichotokea ni kitu kikubwa na wako tayari kuzingatia kuchukua hatua zinazohitajika.

 Vereidigung von Präsident Bah Ndaw in Mali

Wasiwasi iwapo serikali ya mpito itafanikiwa
Matukio hayo yamezua wasiwasi iwapo serikali ya mpito itaweza kuendelea na mipango yake ya kuandaa uchaguzi mpya kama ilivyoahidi kuwa utafanyika Febuari ijayo. Umoja wa Mataifa umekuwa ukitumia dola bilioi 1.2 kila mwaka kuweka ujumbe wake wa askari wa kulinda amani nchini humo.

Viongozi hao wawili waliapishwa Septemba iliyopita baada ya jeshi la mapinduzi kukubali kukabidhi uongozi kwa serikali ya mpito ya kiraia kufuatia shinikizo la kimataifa.

Jeshi lilikamata madaraka mwezi mmoja kabla ya wanajeshi kuizingira nyumba ya Rais Ibrahim Keita na kufyatua risasi hewani. Baadae Keita aliamuwa kujiuzulu kupitia kituo cha televisheni ya taifa na kusema hatomwaga damu ili aweze kubakia madarakani.

Wanajeshi kisha walijitangaza katika kituo cha televisheni ya taifa kama Kamati ya Kitaifa ya Ukombozi wa Watu na kuahidi kurudisha haraka utawala wa kiraia. Lakini, hatua ya kuwakamata rais na waziri mkuu wa nchi inaonekana kutia shaka ahadi hiyo.

Kukamatwa kwa viongozi hao kulitokea saa moja au zaidi baada ya Baraza la Mawaziri la serikali mpya kutangazwa na kutowajumuisha Waziri wa Usalama wa Mambo ya Ndani Modibo Kone au Waziri wa Ulinzi Sadio Camara, wote wakiwa wanachama wa jeshi la mapinduzi.

Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu kutengwa kwao, lakini hatua hiyo inaashiria kuongezeka kwa mgawanyiko ndani ya serikali ya mpito.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad