.

5/23/2021

Rasmi Ndoa Ya Mobeto, Fred Yanukia


KAMA utakumbuka, mapema mwanzoni mwa mwaka huu, mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Hassan Mobeto alitangaza kwamba, mwaka huu, piga ua, lazima afunge ndoa, lakini sasa ni rasmi, matamanio hayo yameyeyuka, Gazeti la IJUMAA limedokezwa.

Tangazo hilo lilitoka siku ile ya Januari 1, mwaka huu sambamba na kuvuja kwa video ya Mobeto ya kimahaba na mfanyabiashara maarufu Bongo, Bilionea Fred Ngajiro almaarufu Fred Vunjabei, wakati huo, ilisemekana mapenzi yao yalikuwa ni ya moto mno.

 

ILITARAJIWA KUFUNGWA JUNIIlidaiwa kwamba, ndoa hiyo ilitarajiwa kufungwa mwezi Juni, mwaka huu, lakini hadi sasa hakuna dalili zozote.Taarifa za wawili hao kuwa wanatoka kimapenzi zilitikisa vilivyo kwa takriban miaka miwili sasa, kabla ya hivi karibuni kudaiwa kumwagana jumla.

 

LAWAMA KWA MARAFIKI WA MWANAUME

Kwa mujibu wa Mobeto, siku zote katika uhusiano wake wa kimapenzi aliowahi kuingia, amekuwa akiumizwa na mapenzi, lakini yote hiyo ni kutokana na marafiki wa wanaume husika ambao anawatupia lawama zote.

 

Kwa mujibu wa Mobeto, hali hii hutokea kutokana na kitendo cha mwanaume kutegemea zaidi marafiki zake katika kuendesha uhusiano wake wa kimapenzi.

Anasema kuwa, kunakuwa na kitu kidogo tu kimetokea kati yake na mwanaume, lakini mwanaume huyo anakipeleka kwa marafiki zake na kupewa ushauri usiofaa ambao matokeo yake ni kuachana.

 

Anashauri kwamba, kwa mwanamke ambaye anapata mwanaume mpya, ni lazima kutazama aina ya marafiki zake na hao ndiyo watakuonesha kama uhusiano wako utadumu.“Kadiri unapomuomba Mwenyezi Mungu aweze kukubariki mwanaume wa maana, usisahau pia kumuomba Mungu marafiki zake wawe ni watu wenye akili timamu, wao ndiyo bodi ya wakurugenzi wanaokujadili,” anasema Mobeto.

 

TUHUMA ZA USALITI

Kabla ya kupeana za uso huku kukiwa na tuhuma za usalti zinazoelekezewa kwa Mobeto, wawili hao walikuwa wakionekana viwanja kadha wa kadha wakila bata la kiwango cha lami.

 

FRED ALIMPA MOBETO MAISHA

Enzi za ukaribu wao, Fred alidaiwa kumpa Mobeto maisha ya kifahari ikiwemo kumpangishia mjengo wa ghorofa maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar.Mbali na kumpangishia mjengo huo, pia alidaiwa kumnunulia gari jipya la bei mbaya aina ya Toyota Prado na kumfungulia lile duka la nguo za watoto la Mobeto Kids ambalo awali lilikuwa la mwigizaji Wema Isaac Sepetu.

 

Lakini kabla hawajaenda mbali zaidi na kufikia hatua ya kuwa kitu kimoja au kuishi pamoja, ghafla tu inasemekana bundi ametua kwenye ukaribu wao.

Gazeti la IJUMAA limebaini kwamba, hali si shwari kwa sababu tayari Fred amemu-unfollow Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni siku chache baada ya kumposti mtoto wa Mobeto aliyezaa na C.E.O Radio EFM, Francis Ciza ‘DJ Majizo’ aitwaye Fantasy akisema anampenda kinoma.

 

Fred alimuondoa Mobeto kwenye kundi la wafuasi wake wa Instagram baada ya kuposti maneno yaliyosomeka;“Kosa la kucheat (kusaliti) huwa halina dhamana, adhabu yake ni kuachika milele!”

 

UJUMBE WAMLENGA MOBETO

Ujumbe huo ulitafsiriwa kuwa ulimlenga Mobeto ambapo watu walikwenda mbali zaidi kuwa atakuwa amecheat (amemsaliti) na mwanaume mwingine.

 

Wasiwasi ulitanda kwa watu wa karibu wa Mobeto ambao walikuwa wakimtegemea Fred kwa mizinga kwani jamaa yupo vizuri kipesa.Wengine wanamlaumu Mobeto kama kweli alimsaliti Fred na kama alimsaliti kweli, je, alimsaliti na nani?

 

FRED AMKANA MOBETO

Katika majibu yake kuhusu kuachana na Mobeto, Fred anakana kwamba, hajawahi kuwa na uhusiano wa kimpenzi na Mobeto kama ambavyo imekuwa ikivumishwa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Fred anasema kuwa anamheshimu mno Mobeto kama dada yake na mfanyabiashara mwenzake na siyo vinginevyo.Fred anawataka watu waache mara moja kuongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo.“Mimi sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Misa (Mobeto) ila ni rafiki yangu tu kama ambavyo huwa naongea na mastaa wengine.

 

“Wala sijawahi kumfungulia duka kama ambavyo inasemekana, naomba watu waheshimu hilo,” anasema Fred na kuongeza;“Marafiki zangu wa nguvu ukiwataja utaanza na Hamisa kisha utamalizia kwa Frank Knows. Sina uhusiano na Hamisa zaidi ya urafiki wa kawaida na kikazi.”

Fred anasisitiza kwamba, hawezi kuwa na uhusiano na Mobeto kwani yeye na Diamond Platnumz ambaye amezaa na mrembo huyo ni watu wanaoshirikiana kwenye biashara.

 

JINA LA FRED LATRENDI

Jina la Fred limeendelea kutrendi kwenye ulimwengu wa mastaa wa kike Bongo ambapo amekuwa akihusishwa nao, lakini mwenyewe akawa anakana.Mbali na Mobeto, wengine wanaotajwatajwa ni Tunda Mahoteli, Tessy Chocolate, Official Nai, Gigy Money na Amber Lulu.

 

MOBETO AKANUSHA NDOA NA FRED

Kama alivyojibu Fred kuwa hana uhusiano na Mobeto, ni kama waliwasiliana kwani mrembo huyo naye alikanusha uhusiano wao.Mobeto ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, hana mpango wa kuolewa na mtu yeyote kama watu wanavyodhani, badala yake anajipanga kuendeleza biashara zake zikue zaidi.

 

Anasema kuwa, watu wengi wanamtabiria kuwa ataolewa na Vunjabei na mambo mengine kibao, lakini ukweli ni kwamba bado yupoyupo sana na siku ya harusi yake ikifika, watu wote watajua.“Ukweli ni kwamba mimi bado niponipo sana, sina mpango wa kuolewa leo wala kesho kwa sababu nina mambo yangu mengi sana ya kufanya kwa sasa hivyo hayo mambo ni ya kufikirika tu, labda kama wanahisi Fred ndiye atanioa, basi wamfuate ili azungumze vizuri kuhusu nani anamuoa,” alifunga mjadala Mobeto ambaye ni mbunifu wa mavazi ya Mobeto Styles.

Stori; Imelda Mtema, Dar

 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger