.

5/24/2021

RC Chalamila: Nahitaji Busara Kuuongoza Mkoa wa Mwanza

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila amewaomba wakuu wa idara na watendaji wa Serikali mkoani humo kumuazima busara akidai za kwake pekee hazitotosha.

 

Chalamila ametoa ombi hilo leo Jumatatu Mei 24, 2021 wakati akizungumza na watendaji, wafanyabiashara, wakuu wa idara, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo mara baada ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

 

Huku walioudhuria katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya ofisi wakiangua vicheko, Chalamila amesema, “yaani mimi hivi unataka niwe kama mzee Meck Sadick (mkuu wa mkoa mstaafu), akiwa mzee Sadick pale na mimi unataka niwe na busara hivyo hivyo? Mjue kabisa nitakuwa najilazimisha kitu ambacho sipo nacho kabisa! Na hii kitu ni automatic tu.”“Sasa sisi jukumu letu tunafanyaje, sisi kazi yetu ni kufanya mazoezi, nikuazima busara, wakinyang’anya unaazima tena. Sasa wakati mwingine huwa nanyang’anywa kwenye maamuzi mazito nashangaa imetoweka. Hoja ya msingi hapa jitahidini sana kuniazima busara, za kwangu peke yangu nina uhakika hazitatosha,” amesema.

 

Amebainisha kuwa akisema hivyo watu wanadhani anatania na ndio maana wakuu wa mikoa wanawekewa makatibu tawala, wasaidizi na wazee lengo ni kusaidia kupooza na kuyeyusha vinginevyo wanaweza kuharibikiwa.

 

Amesema atafunguwa milango ili apate ushauri kutoka kwa watendaji hao akidai ushauri huo ndio busara anazozisema.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger