RC Kunenge Akanusha Taarifa za Kuondolewa Wamachinga Mjini, Asema Wananchi Wazipuuze

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge amesema hakuna mfanyabiashara mdogomdogo almaarufu Kama Machinga atakaeondolewa Katika Jiji hilo Kama taarifa za uzushi kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinavyodai ambapo amewataka wananchi kupuuzia taarifa hizo.

RC Kunenge amesema Serikali inatambua na kuthamini Mchango wa wamachinga kwenye Mkoa huo hivyo amewataka waendelee kufanya biashara zao kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu.

Aidha RC Kunenge amewataka machinga wasijenge kwenye mapito ya watembea kwa miguu Wala Barabarani kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha usalama wao na Vyombo vya Moto.

Pamoja na hayo RC Kunenge ametoa angalizo kwa Wafanyabiashara wenye utaratibu wa kubeba mitungi ya gesi na majiko yanayowaka na kukatizanayo katikati ya watu na vyombo vya Moto jambo ambalo ni hatari kwa usamama.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE