.

5/21/2021

RC Makalla amaliza ugomvi wa Meya na Mkurugenzi Kinondoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa iliyojitokeza Kati ya Meya wa Manispaa ya kinondoni, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Lana.
Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao cha pamoja kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa na kuwakutanisha Meya na Mkurugenz wa Manispaa ya Kinondoni.

Makalla amewataka Viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za Wananchi.

Kwa upande wa Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Wananchi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger