Ripoti ya Mapinduzi Balama Yanga ipo Hivi…

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi anatarajiwa kujiunga na wenzake katika mazoezi ya pamoja hivi karibuni, ambapo tayari nyota huyo ameanza program maalum ya mazoezi mepesi baada ya kupona jeraha la enka alilolipata Juni, mwaka jana.

 

Balama alipata jeraha hilo katika mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda, Juni mwaka jana, na kufanyiwa upasuaji mara mbili hivyo kuwa nje ya uwanja kwa miezi nane.

 Hapo awali timu ya madaktari waliomfanyia upasuaji kutoka Afrika Kusini walimpa muda wa wiki tano ambazo tayari zimemalizika na hivyo kumpa ruhusa ya kuanza mazoezi mepesi kabla ya kujiunga na wenzake.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kuhusiana na Mapinduzi Balama niwaweke wazi kuwa, tayari amekwishapona na anatembea bila usaidizi wa magongo, lakini pia tayari ameanza programu ya mazoezi mepesi ya kukimbia ambayo amepewa maalum na timu yetu ya madaktari ili kurejea katika hali yake ya kawaida.

 

“Licha ya kupona kwa asilimia kubwa lakini, bado hajawa tayari kucheza, na kutokana na ukubwa wa jeraha alilolipata hatuhitaji kumuharakisha ili kuepuka madhara zaidi.”

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE