Sababu ya ongezeko la mstuko wa moyo “heart attack” katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan duniani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





  Katika mwezi huu wa Ramadhan familia nyingi nchini na duniani kwa jumla kuna  nchi ambazo  raia wake wanafunga  saumu hii tukufu kama nguzo moja kati ya tano za kiislaam. Chakula cha jioni au kama kinavyojulikana IFTAR/FUTARI mbali ya kuwa na aina mbali mbali za vyakula bali pia huwa ni vingi kuliko siku za kawaida.
 

Kula futari nyingi kipindi cha magharibi sio tu kutafanya wafungaji na waalikwa wengine kuongezeka uzito mwezi huu wa Ramadhan bali kwa wa wale walaji  ambao wana matatizo mbali mbali ya moyo kama shinikizo la damu la juu (High Blood Pressure), moyo dhaifu (heart failure), moyo uliopanuka (Dilated Cardiomyopathy), mishipa/mirija ya moyo iliyoziba (coronary artery disease CAD)  wanaweza kupata matatizo ya kiafya . 

 

Ulaji wa chakula  kingi kunaweza kuchochea mstuko wa ghafla wa moyo  (trigger heart attack).  Mstuko wa moyo unasababisha mamilioni ya watu kupoteza maisha kila mwaka duniani.  Kila mwaka vifo hivi vinaongezeka zaidi duniani kipindi hiki cha  Ramadhan na wakati wa sherehe mbalimbali kama vile Krismasi, Pasaka na Mwaka mpya.

 

Kwanini vifo vinavyotokana na mstuko wa moyo vinaongezeka kipindi cha Ramadhani?

 

Tafiti zinaonyesha kipindi kama hiki cha Ramadhani vifo vinavyotokana na  mstuko wa moyo  huongezeka mara nne (4) zaidi.  Kuna sababu kadhaa zinazoweza sababisha kuchochea mstuko wa moyo. Sababu hizo ni:

 

1.     Unapokula chakula kingi mpaka kuvimbiwa wakati wa kufuturu/iftar au wakati wa daku ,tumbo la chakula linapanuka ili kupokea chakula hicho hii itapelekea damu mwilini kujipanga upya kwa kutoa damu nyingi kutoka kwenye moyo kuelekea/ kupelekwa “redistribution”kwenye njia ya chakula “Digestive System” ili kusaidia kusaga “digest” chakula kingi kilicholiwa nyakati za futari/daku.  

 

Hali hii ikimkuta mlaji ambae ana tatizo lake la moyo au pressure la/ya siku nyingi/zamani (kwa mfano mirija au mishipa yake ya damu ya moyo  imeziba kidogo au sana)  huu mbadiliko wa mwendo wa damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye tumbo ndio unapelekea kuchochea “trigger heart attack” ambayo itasababisha mstuko wa moyo na athari zake.

 

2.     Tumbo lililojaa kutokana na  ulaji wa chakula kingi sana husababisha moyo kwenda mbio “palpitation” na/au mapigo kutokwenda sawa sawa “irregular heartbeats” hii pia huchochea mstuko wa moyo na wengine kupata kiarusi “stroke”.

 

Ni muhimu watanzania kufahamu  kuwa:

1.     Magonjwa ya moyo yanaongoza duniani kwa kusababisha vifo ukilinganisha na magonjwa mengine yeyote.

2.     Zaidi ya watu millioni 18 hufariki duniani kila mwaka kwa sababu ya magonjwa ya moyo hii ni asilimia 31% ya vifo vyote duniani. Kati ya hivi vifo vya moyo asilimia 85% vinatokana na mstuko wa moyo “heart attack”.

3.     Robo tatu  (3/4) ya vifo hivi vya moyo vinatokea kwenye nchi zenye uchumi mdogo au uchumi wa kati (low/middle income countries).

4.     Asilimia kubwa > 80% ya magonjwa ya moyo yanaweza kukingika (prevented) kwa mfano kuacha uvutaji wa sigara, kula vyakula bora na kwa kiasi (kumbuka bibi zetu walikuwa wanasema usile mpaka uvimbiwe), kupunguza uzito, kufanya mazoezi, kupunguza unywaji wa pombe nk.

5.     Wale waliogundulika na matatizo ya moyo, BP kuwa juu, kisukari, uzito mkubwa “overweight na obesity” kufuata masharti ya madaktari wao.

 

Ushauri:

1.     Ukiona dalili za tatizo la moyo kuchoka kuliko kawaida “fatigue”, shida ya kupumua sawa sawa, kiungulia/maumivu ya chembe “heartburn” na maumivu kifuani. Tafadhali tafuta kwa haraka ushauri wa daktari.  Dalili hizi wakati mwingine  haziwezi kuondoka zenyewe.

2.     Tufungue funga zetu au tule kwa kiasi hasa tule vyakula vyenye protein nyingi kuliko wanga mwingi na hili hasa kwa wale wenye matatizo ya moyo kabla ya mfungo au yamengundulika mwezi huu. Kupunguza vyakula vyenye sukari nyingi.

 

Ushauri huu wa ulaji  wa chakula nimeutoa kwa kila mtanzania.

 

Ramadhan Kareem.

 

Profesa Mohamed Janabi MD.,PhD.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo

Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad