Sakata la BASATA na wasanii kuamuliwa jumamosi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) Mei 1, 2021 wameanza kutumia sheria ya kuzikagua nyimbo zote mpya za wasanii kabla ya kupelekwa kwenye Radio au TV nchini ambapo utaratibu huo mpya unamlazimu msanii kusubiri BASATA ipitishe wimbo wake na akabidhiwe cheti kisha wimbo upelekwa redioni.
Wasanii wengi kwa asilimia kubwa pamoja na wadau wa burudani wameonesha kutopendezwa na sheria hiyo na kutaka BASATA iachane na huo utaratibu au itafute utaratibu mwingine wa kudhibiti nyimbo zisizo na maadili lakini sio huu, sasa baada ya yote hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amejitokeza na kuongea yafuatayo.

“Nimefikishiwa maoni mengi na Wadau mbalimbali kuhusu agizo la Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuhakiki kazi za muziki kabla hazijatoka na inaonekana BASATA wanaona ni njia ya kuboresha kazi na kulinda maadili”

“Wadau nao wana hoja kwamba huko ni kuleta urasimu usio na lazima, tutalimaliza hilo hivi siku ya Jumamosi Mei, 8 2021. Waziri wetu Innocent Bashungwa na mimi tutakaa kuwasikiliza BASATA na Wawakilishi wa Wasanii hoja kwa hoja kisha tutatoa uamuzi wa papo kwa hapo, hili limeisha” – Dkt. Hassan Abbasi


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad