Sarah Amkomesha Harmonize

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


WAKATI akigulia majeraha ya kutemwa na mpenzi wake, Kajala Masanja, Msanii Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ameendelea kupata pigo lingine baada ya aliyedaiwa kuwa mkewe Sarah Michelotti kumrusha roho na kidume mwingine.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki chache zilizopita Harmonize kutaka maoni ya mashabiki zake iwapo amrejee Ex yupi kati ya Jacqueline Wolper na Sarah.

 

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Harmo aliwauliza mashabiki zake amrejee nani huku majibu ya mashabiki wengi wakimtaka amrejee Sarah kwa kuwa ndiye aliyeonekana kumbeba Harmo katika nyanja nyingi hususani kifedha.

 

MAMBO SI MAMBO
Wakati mashabiki wakisubiri majibu ya mikito ya Harmo kwa Sarah, hali imebadilika baada ya Sarah kumuanika mwanaume anayemrusha roho kwa sasa.

 

Sarah ambaye anasifika kwa vijembe na mipasho katika akaunti yake ya Instagram, alibandika picha ya jamaa huyo wakiwa katika mahaba mazito kifuani kwake hali iliyowafanya mashibiki wapigie mstari kuwa anamkomesha Harmo.

 

Aidha, Sarah kupitia akanunti yake, amekuwa akibandika picha na kuandika jumbe mbalimbali kuwa yeye ‘mwanamke wa shoka, hawezi kuchuja,’ pamoja na maneno mengine ambayo yote mashabiki wanayatafsiri kama yanalenga kumkomoa Harmo.

 

Sarah na Harmo ambao walidaiwa kufunga ndoa mwaka 2019, wawili hao walianza kuonesha dalili za penzi lao kuingia shubiri baada ya kuibuka tuhuma kuwa Harmo alibanjuka na mrembo mwenye umbo matata Bongo, Nicole Joyberry Mbaga.

 

Wakati taarifa hizo za Harmo kufumwa na Nicole hazijapoa, Disemba mwaka jana mambo yalizidi kuwa moto baada ya Harmo kumwanika mwanawe aliyedai kuzaa na mrembo Nana Shanteel. Hali hiyo iliibua tafrani na wawili hao kudaiwa kutengana kisha Harmo kuhamia katika penzi la Kajala.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad