Sendiga Asema Hana Kinyongo na Waliomfanyia Vurugu

Mkuu wa Mkoa wa Iringa mteule Queen Sendiga, amesema kuwa yeye hawezi kuyabeba mambo yaliyotokea wakati wa kampeni na kuwa nayo hadi leo, kwa kuwa kwenye kampeni kunafanyika mambo mengi ambayo huishia huko huko.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 17, 2021, alipohojiwa kuhusu tukio la kuvunjiwa kioo cha gari alilofanyiwa na baadhi ya vijana wa mkoa wa Iringa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ambapo yeye alikuwa ni mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha ADC.

Swali "Kuna mahali nadhani ni Iringa walitaka kukupiga wakukuvunjia kioo cha gari, sasa unaenda kuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa watu wasije wakakoma wale walifanya mzaha mzaha," aliuliza Paschal Mayala mtangazaji mwalikwa.

"Hizo zilikuwa kampeni zilishamalizika, hayo yatakuwa ni mambo ya kipuuzi sasa na kwenye kampeni huwa kuna mambo mengi mno, huwezi ukaondoka na mambo ya kwenye kampeni ulale nayo na uamke nayo, hayo yalishamalizika muda mrefu," alijibu Queen Sendiga.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE