Serikali Yakanusha Kuachia Wafungwa wa Kisiasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Serikali ya Tanzania imetaka kupuuzwa kwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni na katika chombo cha habari kutoka nchi jirani ya Kenya zinazosema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameachia wafungwa wa kisiasa.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan hawezi kuingilia mahakama na kwamba Tanzania haina wafungwa wa kisiasa. Amesema kuwa hatua mbalimbali za kisheria zinafuatwa, kufuatia usambazwaji wa taarifa hizo za uongo.

 

“Kuna jambo tumeona tulitolee ufafanuzi. Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa 23. Siyo kweli. Rais hahajazungumza suala hilo. Pili, nchi yetu haina wafungwa wa kisiasa. Watanzania wapuuze taarifa hizo.”

 

“Hiki chombo cha Habari cha nchi jirani, nisingependa kukitaja, tunaamini wataomba radhi na kufuta taarifa hiyo. Tayari ofisi yetu ya Ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wmepotosha,” amesema Msigwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad