Serikali yamjibu anayetaka manabii waanze kufufua

  


Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi imesema kuwa ipo tayari kukutana na manabii wanaodai kuweza kufufua wafu ili iweze kuwaelimisha na kuwaelekeza kuwa mwenye uwezo wa kuchukua na kurejesha ni Mungu pekee.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Mei 17, 2021, Bungeni Dodoma, na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamza Chilo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe kupitia Chama cha ACT-Wazalendo Khalifa Mohamed Issa, aliyehoji umuhimu wa serikali kukutana na wale manabii wanaodai kuweza kufufua wafu ili waweze kuwafufua wapendwa wao.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE