.

5/29/2021

Simba na Namungo Kukupiga Leo

 KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, amefunguka kuwa moja ya malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha wanapata matokeo katika kila mchezo wa ligi, ukiwemo mchezo wao ujao dhidi ya Namungo baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inarejea tena kwenye ligi baada ya safari ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali ambapo leo Jumamosi watakuwa uwanjani kucheza dhidi ya Namungo mkoani Lindi.


Timu hiyo ambayo inaongoza ligi kwa pointi 61 sawa na Yanga, inayokamata nafasi ya pili lakini wakiwa na tofauti ya mabao na mechi (Yanga wako mbele kwa mechi nne).


 Gomes amesema kuwa kwa sasa watawekeza nguvu zao zote katika mechi zao za ligi kwa kuanza na Namungo kwa kuwa wanataka kuona wanafanikiwa kutetea ubingwa wao kufuatia kuondolewa kwenye michuano ya kimataifa.


“Kitu pekee kwa sasa ni kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao ili tuone kwa namna gani tunaweza kufika mbali ya tulipoishia, nguvu yetu tunaipeleka kwenye mechi zetu za ligi kwa kuhakikisha tunashinda, tukianzia mechi yetu dhidi na Namungo, maana ndiyo itakuwa ya kwanza katika ligi.


"Unajua mashindano si rahisi wala si timu ya kawaida kwa kuwa kila timu inakuwa imejiandaa kupambana kwa kuhakikisha wanapata matokeo, hivyo tunaenda kucheza ugenini tukiwa na lengo moja pekee la kuhakikisha tunashinda ili kujiweka kwenye wakati mzuri wa kutetea ubingwa wetu msimu huu,” amesema Gomes.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger