Simba ndiyo basi tena ligi ya mabingwa ?

 


Baada ya timu ya Simba SC kufungwa bao 4-0 na Kaizer Chief katika mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa Afrika.

 

Mjadala mkubwa umeibuka juu ya hatma ya Simba katika mashindano haya,hususani majaliwa yake ya kusonga mbele hasa ukifuatia matokeo yaliyopatikana katika mchezo wa awali katika uwanja wa FNB mjini Johannesburg.


Simba atakuwa mwenyeji wa Kaizer Chiefs tarehe 22/5/2021 katika uwanja wa hayati Benjamin Mkapa jijini Dar-es-Salaam,lakini mjadala uliopo je wekundu hao wa msimbazi watafanikiwa kusonga mbele kwa maana ya kupata ushindi wa juu ya 4.


Yote yanawezekana japo inahitaji nguvu nyingi na maarifa makubwa kubadili matokeo hayo ya mkondo wa kwanza ,kushinda chini ya mabao matatu hakutaleta maana , Simba amelazimika kushinda tu ushindi mkubwa ili iweze kusonga mbele.


Simba wanajivunia rekodi ya mwaka 1979 waliofanikiwa kupindua matokeo dhidi ya Mfulira Wanderers ya Zambia baada ya kufungwa bao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza Dar-es-Salaam,na kisha kupata ushindi wa 5-0 katika mchezo wa mkondo wa pili kwao

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE