Simba yatoa tamko kughairishwa kwa Derby yao na YangaKlabu ya Simba inapenda kutoa tamko kuhusu kuahirishwa kwa mchezo wake dhidi ya Yanga, uliokuwa ufanyike jana Mei 8, 2021

Mnamo majira ya saa saba mchana, tulipokea simu kutoka Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikituelekeza kuhusu mapendekezo ya kuahirishwa kwa mchezo huo kutokana na maelekezo ya Serikali. Muda mfupi baadaye , tulipokea taarifa rasmi ya kimaandishi juu ya uamuzi huo kutoka kwenye mamlaka hizo zinzazosimamia mchezo wa soka nchini.

Pamoja na kusikitishwa na uamuzi huo, sisi kama Klabu tulikubali hasa kwa kuzingatia kwamba wote tunafanya shughuli zetu chini ya mamlaka hizo na tunaamini kwamba kama wameamua kuchukua hatua hiyo basi wanazo sababu za msingi hatukuhoji. 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE