5/05/2021

Simbachawene: Kitambulisho cha Nida Hakihalalishi Kuwa Raia wa TanzaniaWaziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, amesema kuwa na kitambulisho cha Utaifa (NIDA) hakuhalalishi Mtu kuwa Raia wa #Tanzania.


Akiwa Bungeni, Simbachawene ameeleza Uraia wa Tanzania una #Sheria ya Uraia na una mchakato wake hivyo kitambulisho cha NIDA ni kwa ajili ya kuwatambua tu Wananchi na hutolewa hata kwa Wakimbizi na Wahamiaji wakazi.


Ameongeza “Ukipata kitambulisho hiki sio mwarobaini kwamba wewe umeshamaliza sasa hutaulizwa hapana, utaulizwa na utanyang’anywa hicho kitambulisho kama tukigundua wewe sio Raia wa Tanzania”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger