Solskajer Hafurahishwi na Kampeni za Gary Nevile


IMEELEZWA kuwa, Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer na benchi lake la ufundi hawafurahishwi na kitendo cha beki wa zamani wa timu hiyo Gary Nevile kuendeleza kampeni zake za kupinga umiliki wa Familia ya Glazer kuhusu klabu hiyo.

Gary akiwa ni mchambuzi wa soka la kituo cha Sky TV amekuwa mstari wa mbele kupinga familia hiyo kumiliki timu hiyo.Mashabiki wa United wamekuwa hawapendi jambo hilo na hivi karibuni waliandamana kupinga suala hilo la umiliki wa familia hiyo.

 

Maandamano ya mashabiki hao yalifanya mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool kuyeyuka mazima jambo ambalo limeongeza mzigo mzito kwa timu yake kuwa na mechi nyingi mfululizo.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE