5/16/2021

Tunaweza kubadili matokeo – Kocha Didier Gomes
Kocha wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Simba SC, Didier Gomes amesema kuwa kwenye mchezo wa Mpira wa Miguu jambo lolote linawezekana hivyo anaamini wanayonafasi ya kuweza kubadili matokeo kwenye mchezo wao unaofuta wa Michuano ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs baada ya hapo jana kupokea kipigo kitakatifu cha magoli 4 – 0 nchini Afrika Kusini“Jambo lolote linawezekana kwenye mpira, hatujafurahia matokeo lakini bado tuna matumaini, ni muhimu sana kuamini kwamba tunaweza kubadili matokeo. Lakini kama tunataka kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano lazima tuwe bora zaidi.”- Kocha Didier Gomes.

Simba SC ambayo ndiyo timu pekee inayowakilisha nchi kwenye michuano ya CAF hapo jana ilipokea kipigo kibaya cha magoli hayo 4-0 baada ya dakika 90 kukamilika.

Mchezo wa marudiano Simba atamkaribisha Kaizer Chiefs pale machinjioni katika Uwanja wa Mkapa tarehe 22 ya mwezi huu 2021.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger