.

5/26/2021

Ufalme wa Hanscana Kama Video Director Umefikia Mwisho - Amekuwa Mwenye Hofu Sana Sasa Hivi

 


Tasnia ya utengenezaji wa video za wasanii wa Bongo fleva imeanza kitambo sana.


Kumekuwa na Directors wengi lakini mapinduzi ya video yamekuwa yakifanywa na Directors ili kuanzisha either trend mpya au Directors wenyewe kulazimika kukua baada ya wasanii kutaka video zenye ubora.


Kuna wakati Adam Juma ( Next Level ) alifanya mapinduzi makubwa sana kwenye hii tasnia lakini ghafla akatokea Nisher ( kijana wa Arusha )


Ujio wa Nisher kwenye tasnia uliwafanya wasanii wengi kufunga safari kuelekea Arusha kwaajili ya video.


Uwepo wa Nisher ndio uliomzalisha Hanscana na Khalfan.


Zaidi ya asilimia 80 ya video za wasanii wakubwa bongo zimekuwa zikifanywa na Hanscana kwa hapa Tanzania.


Fast foward sasa hivi, kumekuwa na Directors kibao wanaofanya vizuri kiasi kwamba choices zimekuwa nyingi.


Kuna Ivan, Elvis, Kenny, Msafiri, etc


Na kibaya zaidi wasanii wengine wamekuwa wakianzisha kama ilivyo kwa studio zao wenyewe, kampuni zao za video shooting.


1- Wasafi wana Zoom Extra


2- Kondegang ( tetesi wanamiliki Redshot )


Na hakuna asiyejua kuwa hawa ndio wasanii wenye kazi nyingi za video na malipo yasiyo na shaka.


Hali hii naona imesababisha Hanscana apate "Mhaho" kutokana ushindani uliojitokeza. Na asipojiangalia atapotea kama Adam Juma halafu ajifanye kastaafu

Jamii Forums

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger