Ujenzi Bwawa la Nyerere wafikia asilimia 51

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa, utekelezaji wa mradi mkubwa wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere kwenye maeneo muhimu umefikia asilimia 51.5 kwa sasa.
Dkt. Kalemani ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya kukagua hatua za utekelezaji mradi huo wa Julius Nyerere akiambatana na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoka Misri, Dkt. Assem Elgazzar.

Dkt. Kalemani ameyataja maeneo ya ujenzi huo yaliyokamilika kwa asilimia hizo kwa ujumla wake kuwa ni, ujenzi wa tuta kuu, ujenzi wa wa jumba la kuendeshea mitambo, ujenzi wa njia za kupeleka maji kwenye mitambo ya kufua umeme pamoja na kituo cha kupokea na kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400.

“Mbali ya utekelezaji wa mradi kufika hatua hiyo lakini pia hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa shilingi trilioni 2.4 kulingana na mpango kazi,” Dkt. Kalemani.

Awali akielezea maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwa niaba ya Mhandisi Mkazi, Mhandisi Lutengano Mwandambo kutoka TECU amesema timu ya wataalamu kutoka Tanzania imeenda kukagua utengenezaji wa mitambo ya kufua umeme itakayotumika katika mradi huo.

Aliongeza kuwa, kufikia mwezi Novemba mwaka huu kazi ya kujaza maji kwenye bwawa itaanza ambapo itakwenda hadi Aprili mwaka 2022 ambapo kiwango cha maji kitakuwa kimefikia kina cha 163 juu ya usawa wa bahari, kiwango ambacho kinatosha kuanza kufua umeme.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad