Vanessa: Naishi Maisha Yangu

MWANADADA anayejua kutupia pamba vilivyo ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema kuwa anaishi maisha yake na siyo maisha wanayotaka watu aishi.

 

Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, mwanadada huyo ambaye kwa sasa makazi yake yapo nchini Marekani aliendelea kusema kwamba, siku hizi maisha yamekuwa mafupi hivyo ukiendekeza na kusikiliza maneno ya watu utakufa mapema, ndio maana alipogundua hilo aliamua kuziba masikio na kuishi yale maisha anayoona kwake yanafaa.

 

“Unajua siku hizi maisha ni mafupi sana hivyo tunatakiwa kufurahia maisha na sio kukaa na vinyongo moyoni, ndio maana huwa siruhusu watu waendeshe maisha yangu kabisa, isipokuwa mimi tu, yaani kwa ufupi napenda kuishi maisha yangu” alisema Vee. wa kolabo, ataanza na wasanii wa Afrika Mashariki.“

 

Huu mwaka utakuwa ni mwaka wa kufanya kolabo kama yote, nitaanza na wasanii wa Afrika Mashariki, kwa hiyo mashabiki wakae tayari,” alisema Bright ambaye miaka michache iliyopita aliweza kufanya kolabo na msanii wa kike wa Bongo Fleva, Faustina Charles

STORI: MEMORISE RICHARD


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE