.

5/28/2021

Vee Money & Rotimi Waachia Kitabu Chao Kipya ‘Swahili 101’

MSANII wa Bongo Fleva, @vanessamdee ‘Vee Money’ na mpenzi wake @rotimi wametayarisha kitabu chao cha Lugha ya Kiswahili na kukitambulisha rasmi hii leo kupitia mtandao wa Instagram.

 

Kitabu hicho wamekipa jina la “Swahili 101” ambacho kimezinduliwa na wapenzi hao ikiwa ni sehemu ya kukikuza Kiswahili kimataifa na kujifunza kwa wasioijfahamu lugha hii kwa ufasaha.

 

Vee Money amefanya haya baada ya @vanessamdee kumfundisha mwandani wake @rotimi Lugha hiyo na sasa anaweza kuzungumza vizuri baadhi ya maneno ya Kiswahili.

 

Wakitangaza kitabu hiki kupitia mitandao ya kijamii, wamesema kitabu kitauza kwa dola za Kimarekani $9.99 ambazo ni sawa na Tsh 20,700/= na kitapatikana kupitia mtandao wa Amazon.

 

Pia, katika taarifa yao hii @rotimi ameweka wazi kuvutiwa sana na Lugha ya Kiswahili aliyofundishwa na mpenzi wake @vanessamdee.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger