Vibanda Katikakati ya Jiji Kuondolewa Kabla ya Mei 18Waliojenga vibanda vya biashara katikati ya Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kuviondoa kabla ya Mei 18, 2021

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amesema hawajazuia Wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao, bali wanatakiwa wauze bidhaa kwenye meza wakimaliza waziondoe na kuacha maeneo wazi

Amebainisha kuwa Sheria ya Mipango Miji hairuhusu kujenga vibanda, hivyo amewataka Wafanyabiashara kutii agizo hilo kabla ya muda uliopangwa


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE