Wakaazi wa Goma waanza kurudi majumbani baada ya kukimbia volkano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wameanza kurejea katika majumba yao kutokana na hali ya ukosefu wa chakula katika maeneo waliyokimbilia. 


Kwa sasa mitetemeko midogo ya ardhi na ongezeko la joto ndiyo mambo yanayoendelea kushuhudiwa licha ya moto uliotokana na volkano kuonekana kuanza kupungua. Maelfu ya watu wameyakimbia makaazi yao baada ya mlima Nyiragongo kulipuka usiku wa kuamkia leo. 



Mara ya mwisho mlima huo kulipuka ilikuwa Januari 17 mwaka 2002 ambapo zaidi ya watu mia moja walipoteza maisha na tope la Volcano lilienea karibu Goma mashariki yote ikiwemo nusu ya eneo la kutua ndege katika uwanja wa ndege wa mji huo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad