Wakazi Atema Nyongo "BASATA Ifutwe Tuanze Upya"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ni wiki yenye muendelezo wa mjadala mpana wa kutoa maoni na upembuzi kuhusu kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa - BASATA na wajibu wake katika sanaa ya taifa letu.

Rapa Wakazi amekuwa sehemu ya wachangiaji wa moja kwa moja ambapo jana alisema anaona BASATA inafaa kufutwa na tuanze upya. Kwenye mahojiano na EMPIRE ya @efmtanzania Wakazi alianzisha hoja hiyo kwa kusema haoni mchango chanya wa BASATA hadi sasa kwa wasanii na sanaa kwa ujumla. Aliungwa mkono na wachangiaji wenzake akiwemo @nikkwapili na mtayarishaji @hermyb

Kuna nyanja ambazo alizigusa kama; Kanuni zimelenga kumdhibiti msanii na sio kudhibiti haki za kazi ya sanaa kwa hivyo BASATA wanafanya kazi nje ya mpango wa Serikali ambao unaeleza kwa mapana kwenye kukuza sanaa, kuongeza ajira kwa asilimia 2.4 na pia kuchangia pato la taifa kwa asilimia 1 ifikapo mwaka 2025. Sababu kubwa nyingine aliyoitoa ni kwamba wasanii wafanye kazi zao kwa uhuru lakini kwa kuzingatia kanuni (guidelines) ambazo zinatakiwa kutolewa kwa vyombo vya habari kwa ajili ya kuchuja maudhui yanayokwenda hewani.

Una maoni gani kuhusu hili, tuachie comment yako?

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad