Watu 30 Wafariki Kwenye Mlipuko wa Bomu

 


ZAIDI ya watu 30 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea nje ya shule ya wasichana katika eneo la mji mkuu wa Afghanistan wa Kabul.

Mlipuko huo umetokea katika wilaya ya magharibi mwa Kabul ya Dasht-e-Barchi, wakati wakaazi wengi walipokuwa wakifanya manunuzi ya kuelekea sikukuu ya Eid-al-Fitr.

Eneo hilo linakaliwa kwa kiasi kikubwa na jamii ya washia wa Hazara na limekuwa likilengwa na wanamgambo wa Kisuni.

Mlipuko huo unatokea wakati Marekani ikiendelea kuviondosha vikosi vyake vya usalama vilivyosalia kutoka Afghanistan, nchi iliyokumbwa na machafuko.

Juhudi za kutafuta amani kati ya serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban kumaliza vita vya miongo kadhaa zimekuwa zikilegalega, kundi la Taliban limekana kuhusika na shambulizi hilo.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE