.

5/30/2021

Waziri Mkuu Uingereza afunga ndoa
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amefunga ndoa na Carrie Symonds katika sherehe ndogo iliyofanywa  kwa siri huko Westminster Cathedral.


Boris anakuwa waziri mkuu wa kwanza kufunga ndoa akiwa anaitumikia ofisi ikiwa imepita takribani miaka 200 tangu kutokea kwa tukio la aina hiyo.Wawili hao waliofunga ndoa jana Jumamosi Mei 29, 2021 huku Waziri Nadhim Zahawi akisema  hakuhudhuria sherehe hiyo lakini amewatakia kheri katika ndoa yao."Ninadhani ni jambo la kufurahisha kwa wote wawili kuweka nadhiri zao za ndoa, ninawatakia kila la kheri," amesema Zahawi.Ingawa Boris alishawahi kufunga ndoa mara mbili,  Kanisa Katoliki linaruhusu watalaka kufunga ndoa nyingine iwapo viapo vya ndoa za zamani vililiwa nje ya kanisa hilo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger