Wema na Zari, Vita Imenoga

advertise hereILIANZA kama masihala tu hivi lakini sasa hivi mambo yametaradadi kati ya muigizaji Wema Sepetu na mrembo kutoka pande za Sauz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wanapigana vijembe ile mbaya.

 

Awali, ishu ilianza mara baada ya muigizaji Wema kumzungumza vibaya Zari kwenye moja ya mahojiano yake na kisha Zari kujibu kwa maneno ya kebehi katika posti ya mmoja wa mashabiki wa mastaa hao.

 

Shabiki huyo anayejiita Therealcathe_tz alimchokoza Zari kwa kuandika maneno haya:“Zari wee mbwa wako hajapotea kama wa Wema? Halafu Wema alikujibu vibaya Boss lady.

 

”Zari akajibu hivi:“It’s ramadhan na natoa msaada. He could use some free food, naona kabakisha kichwa tu. Hiyo ni njaa let her eat some food she will be fine.”Hapo ndipo msala ulipokolezwa mitandaoni kwa watu kusambaza ujumbe huo wa Zari ambapo mashabiki wa mastaa hao walianza kurushiana maneno makali.Upande wa mashabiki wa Wema walimponda Zari huku wale waliokuwa upande wa Zari wakimponda Wema.Wema alipoona mjadala umekuwa mkubwa, ikabidi aingie kutuliza hali ya hewa kwa kuandika ujumbe wa kumpuuza Zari.

 

“Kugombana na watu wazima ni kujitafutia laana na mimi nina heshima sana kwa wakubwa zangu pia msikivu…nafanyia kazi ushauri,” aliandika Wema.Huku na huku, Zari alirudi kwa staili nyingine kwa kumponda zaidi Wema.“Wanajiona wasichana wadogo umri umeenda mafanikio wamebakisha vichwa ka boflo.

 

”Zari na Wema wamewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa nyakati tofauti. Zari alibahatika kuzaa naye watoto wawili huku Wema yaye akiwa hajabahatika.

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE