5/15/2021

Wolper Awa Mbogo Kisa Mpenzi Wake

MSANII wa filamu Bongo Jacqueline Wolper hivi karibuni amesema kuwa sbabu kubwa inayomfanya awe Mbogo kwenye uhusiano wake wa kimapenzi pindi anapogundua mwanaume wake amemsaliti huwa ni yeye kuwa mwaminifu.

 

Akichezesha taya na Ijumaa mwanamama huyo ambaye kwa sasa amefanikiwa kupata mtoto wa kiume aliyempa jina la P, alisema kuwa mara nyingi anapokuwa na mtu huwa anajitahidi sana kuwa mwaminifu kwake kwa kutomsaliti na mwanaume yoyote yule, sasa inapotokea mwanaume wake akawa na mwanamke mwingine ndio hubadirika na kuwa Mbogo.

 

“ Mimi nikiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume, huwa siwezi kumsaliti kabisa, mara nyingi nakuwa mwaminifu kwake na kumsikiliza kwa kila hali, lakini inapotokea yeye ananiendea ndivyo sivyo mara sijui naanza kuona ana dalili zote za kunisaliti hapo ndio huwa nakuwa Mbogo kwa sababu sitaki mchezo kabisa,” alisema Wolper.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger