.

5/26/2021

Yanga Watoa Tamko Usajili wa Ajibu

BAADA ya tetesi nyingi kuzagaa za kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu kusajiliwa na Yanga, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kutoa tamko rasmi.

 

Juzi tetesi zilizagaa za nyota huyo kusajiliwa kinyemela na mmoja wa mabosi wa Yanga kwa dau la Sh 45Mil kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Ajibu ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huku tetesi zikizagaa kuwa Simba haina mpango wa kumuongezea mkataba mwingine.

 

Akizungumza na Championi Jumatano,Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Hassan Bumbuli, alisema kuwa, ni ngumu kwa hivi sasa kufikiria kumsajili Ajibu kutokana na malengo waliyonayo katika kuelekea msimu ujao.Bumbuli alisema kuwa, kwa hivi sasa uongozi wa timu hiyo hauna mpango wa kumsajili kiungo huyo kutokana na kukosa vigezo vya kuichezea timu hiyo.

 

Aliongeza kuwa wapo baadhi ya wachezaji ambao kocha Nasreddine Nabi aliwapendekeza na Ajibu hayupo katika orodha hiyo, hivyo ni ngumu kwa wao kumsajili.

 

“Tunafahamu kila kitu kinachoendelea kuhusiana na huyo Ajibu, ukweli ni kwamba ni uzushi wenye lengo la kumtengenezea soko katika klabu nyingine baada ya timu yake kupanga kuachana naye.“

 

Kama uongozi hilo suala la Ajibu halipo kwenye meza yetu na usajili wake hatujawahi kuuzungumzia, licha ya kuwepo baadhi ya wachezaji waliopo katika mipango yetu,” alisema Bumbuli


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger