Yanga yatinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC)

advertise hereTimu ya Yanga SC wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke dakika ya 25 na 57 na kwa ushindi huo, Yanga SC watakutana na Biashara United,Nusu Fainali hiyo itachezwa  katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi. 

Robo Fainali za michuano hiyo,  zitachezwa kesho kati ya Rhino Rangers na Azam FC hapo hapo Kambarage majira ya saa kumi jioni  na usiku Simba SC ma Dodoma Jiji FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE