Zidane ataka historia kabla ya kuondoka Madrid

 


Zinedine Zidane anataka kuondoka Madrid akiwa mshindi wa taji la Laliga, taji moja zaidi la LaLiga litamfanya kuwa kocha wa kwanza wa Real Madrid kushinda ligi mara mbili mfululizo tangu 1989, Hivyo anatamani kuondoka na beji ya heshima. 

 


Taarifa za kocha huyo kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wa kihistoria wa ulaya zimekuja baada ya kupata ushindi wa goli 4 kwa 1 juzi dhidi ya Granada, hivyo zidane atahitaji ushindi katika michezo iliyobaki dhidi ya Athletic club Bilbao usiku wa leo mei 16, na ule dhidi ya Villareal siku ya jumapili ili atimize azma yake.


Huku akitazamia matokea ya kufungwa kwa Atletico Madrid katika michezo yake miwili ya mwisho, dhidi ya Osasuna usiku wa mei 16 na ule wa jumapili dhidi ya Valladolid.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE