Akamatwa akitaka kuwauza watoto wake mapacha, akanunue madawa ya kulevya
Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini amekamatwa pamoja na watu wengine wawili kwa madai ya kujaribu kuwauza watoto wake wawili wachanga pacha, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.Mama huyo anadaiwa kuwa mraibu wa madawa ya kulevya na alijaribu kuwauza watotowake kwa ajili ya ‘kukata kiu uraibu wa dawa”, msemaji wa polisi Yolisa Mgolodela, alinukuliwa akisema.

Mapacha wa siku tano wasichana walipelekwa kwasababu walikuwa na “upungufu wa maji mwilini na utapiamlo”, ilisema polisi.

Washukiwa wanatarajiwa kufika mahakamani kujibu mashtaka ya ulanguzi wa binadamu Jumatatu.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE