AL Ahly na Kaizer Chiefs kukutana fainali Ligi ya Mabingwa Afrika
MABINGWA watetezi, Al Ahly wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia usiku huu Uwanja wa WE Al-Ahly Jijini Cairo nchini Misri.

Mabao ya Ahly yamefungwa na Ali MaĂ¢loul kwa penalti dakika ya 38, Mohamed Sherif dakika ya 56 na Hussein El Shahat dakika ya 60.

Kwa matokeo hayo Al Ahly wanatinga Fainali kwa jumla yaa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita Tunisia. 

Al Ahly sasa itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Wydad Athletic baada ya sare ya 0-0 leo Johannesburg kufuatia ushindi wa 1-0 Jumamosi iliyopita Morocco.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad