Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Azam "Kama si Ubingwa Basi Nafasi ya Pili"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa mipango yao ni kuhakikisha wanamaliza Ligi Kuu Bara katika nafasi mbili za juu katika msimamo ukiwemo ubingwa katika msimu huu.


Azam hadi sasa ipo nafasi ya tatu huku ikiwa na pointi 60 katika msimamo wa ligi ikiongozwa na Yanga yenye pointi 61 huku kinara akiwa ni Simba wenye 67.


Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa timu hiyo, Thabit Zakaria alisema kuwa upo uwezekano mkubwa kwao kupata nafasi ya pili kama watakosa ubingwa wa ligi.


“Maandalizi ya kumalizia mechi zetu zilizobaki bado yanaendelea kama kawaida na lengo letu ni kuhakikisha tunachukua nafasi ya pili kama tutakosa kuchukua ubingwa wa msimu huu.“


Kwa upande wa kikosi kipo salama kambini isipokuwa baadhi ya wachezaji ambao waliumia katika mchezo wa kirafiki Never Tigere na Bryson Raphael lakini pia na Prince Dube ambaye ana malaria,” alisema Zakaria

HAWA ABOUBAKHARI NA FRANK BUNINI, DSJ


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments