.

6/08/2021

Baada ya kusambaa picha zisizo na maadili ikidaiwa kuwa ni Kajala, Mwenyewe atoa tamko zito

 Kufuatia picha iliyosambaa mitandaoni (isiyokuwa na maadili) ikidaiwa kuwa wanaonekana pichani ni Muigizaji Kajala na binti yake Paula, hatimae @kajalafrida amekanusha vikali kuhusishwa na picha hiyo pamoja na binti yake.
Kwenye maelezo yake aliyoyatoa kupitia ukurasa wake wa Instagram (tamko langu) @kajalafrida ameeleza, aliyepichani siyo yeye wala sio binti yake na kamwe hawezi kupiga picha kama hiyo.

"Kumekuwa na picha ikisambaa ikiwaonesha wanawake wawili wakiwa watupu kwenye mkao usiofaa na wanawake hao wameonekana wakitofautiana umri, picha hiyo ikaeditiwa na kuwekwa kichwa changu ama kinachofanana na changu huku watu wakisambaza kwa kusema ni mimi na mwanangu".

"Hata kama nina ushenzi wa namna gani, sijafikia na wala sitafikia huko hiyo ni laana iliyopitiliza sijui waliofanya hivyo wana malengo gani na mimi, sijawahi na sitawahi kupiga picha ya namna hiyo na binti niliyembeba tumboni miezi 9 na kumzaa kwa uchungu" - ameeleza @kajalafrida.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger