.

6/02/2021

Basi la Classic Lapata Ajali, Watatu Wafariki

 


WATU watatu wanahofiwa kufariki dunia huku wengine wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Classic kupata ajali eneo la Buyubi kata ya Didia barabara ya Kahama – Tinde Halmashauri ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumanne, Juni 2, 2021, majira ya 10 alfajiri ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Jijini Kampala nchini Uganda kuelekea Jijini Dar es salaam.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya majeruhi wamesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva kushindwa kuimudu kona ya Didia.

Mkuu wa jeshi la Polisi wilayani Shinyanga, John Kafumu amefika eneo la tukio na kubainisha kuwa taarifa zaidi zitatolewa na Kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger