Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Gari La Mondi Msamiati Uleule

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

MTI wenye matunda ndiyo hupigwa mawe; ni msamiati ambao umekuwa ukijirudia kwenye maisha ya msanii Diamond au Mondi.

Awali Mondi aliponunua gari lake la kwanza la kifahari aina ya Cadillac, ‘chawa wapinzani’ wakasema hana uwezo huo na baadaye kubadili gia kwa kusema msanii huyo amenunua gari chakavu kutoka kwa mtu.

 

Kabla ‘mate’ hayajakauka Mondi ameona “isiwe tabu” kavuta gari jingine jipya aina ileile na kulishusha laivu kutoka kwenye kontena nyumbani kwake Mbezi, jijini Dar.

 

Pengine alitaka kuwaziba midomo ‘chawa’ wapinzani ambao walikuwa wakimbeza mwanzo kwa kuliita gari lake chakavu ambapo kwa sasa aliamua kumenya kitu kutoka kwenye makaratasi huku video ikichukuliwa.

 

Lakini Mondi amejikuta kwenye msamiati uleule wa mti wenye matunda kupigwa mawe, ‘chawa’ wapinzani wakiongozwa na Mwijaku wameibuka tena na kusema: “Jamaa anayafanyia maigizo maisha ya utajiri.”

 

Sasa anafeki vipi maisha wakati jamaa anazidi kupepea kimafanikio kwa kujiunga na familia za wajanja wa mbele kama Jay Z na Dobald Trump ambao wanamiliki ndiga kama yake?

Majibu watakuwa nayo chawa wapinzani ambao wamegeuza mitandao ya kijamii kwa sasa kuwa uwanja wa kumshambulia Mondi kwa vile tu kanunua gari jingine la kifahari.

Jema la kuwambusha wote ambao hawapendi mafanikio ya wenzao ni kwamba, “masikini hawezi kutajirika kwa kumcheka tajiri.”

Post a Comment

0 Comments