.

6/02/2021

Hatimaye Manji Arudi Bongo
IMEELEZWA kuwa mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewasili nchini Tanzania Jumanne, Juni Mosi, 2021 jioni baada ya kukaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa sasa.
Manji alikuwa akitajwa kuwa wakati wowote atarejea nchi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Taarifa zinaeleza kuwa alihojiwa kwa muda kadhaa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wake wa kuingia nchini.

Imeelezwa kuwa baada ya kutoa maelezo yake, aliachiwa baada ya maofisa hao kujiridhisha kuwa Manji ni Mtanzania na anayo haki na uhalali wa kuingia nchini Tanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger