.

6/05/2021

Hatimaye Siri imefichuka, Timu Burnaboy dhidi Ya Diamond PlatnumzDiamond Platnums amechaguliwa kuwania tuzo za BET , akiwa ni yeye pekee tokea pande za Africa mashariki....

Kipengele hcho yupo sambamba na mkali Burna boy tokea Nigeria..!


Kinachoshangaza ni kuwepo Kwa makundi yanayompinga kumpigia Kura kutokea hapa hapa nchini kwake Tanzania mahali ambapo alitakiwa apate support kubwa zaidi ....

Makundi hayo yapo sehemu kuu mbili.


1. Kundi linalompinga Kwa mlengo wa kisiasa likiongozwa na accnt maarufu tokea mtandao wa Twitter ya Kigogo 2014...

Hao sababu zao kuu ni Diamond kutohusika katika kukosoa kile wanachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu nchini... Pamoja na kuwa upande wa chama tawala cha CCM.


2.Kundi linalompinga Kwa chuki na maslahi ya kimziki ... likiongozwa na mtangazaji wa Clouds Mwijaku , na accnt zingine za udaku eg Carry mastory , Jay maudaku, E.fm media n.k ...... in short group lote la konde gang...


Na hili kundi la pili ndo nitakaloliongelea Mimi.....


Bila kupepesa macho mziki wa bongo fleva Una waanzilishi wake na Una wakongwe wake hata hivyo Diamond Platnumz ameunyanyua mziki huu Kwa kiwango cha juu kuliko msanii yyte Yule .....


Kundi hili limekuwa likijihusisha na kumpa support Harmonize , wakiwa na lengo au matumaini ya kuwa huenda ana nyota ya kumpita Diamond Platnumz , ...story zao , post zao na kila kitu wanachokifanya kimekuwa na vimelea au lengo la kumgusa Diamond Platnumz in a negative way..


Hakuna asiyejua kuwa Burnaboy ni mwanamziki hodar Kwa sasa Africa , na wala hahitaji support ya watanzania kuchukua tuzo hyo , tuzo ya BET kuchukua inategemea unajulikanaje international level

Na bila Shaka Burnaboy anajulikana Zaid kuliko Diamond , kismingi Burnaboy kuchukua hyo tuzo ni Jambo la kufikia na Diamond akichukua basi itakuwa ni Jambo la kupongezwa .....


Lakni Kwa nini hawa waswahili wamelivalia njuga Kwa kiwango hcho ......

Iko hvi , kinachowaumiza kichwa supporter wa Harmonize ni namna ya kupenya na kufika mbali kama alivyo boss wake wa zamani Na aliyemtoa kimziki Diamond Platnumz ,


Wanaona kijana wa Tandale amepenya zaidi , na maneno Yao ya uswahili kimsingi hayagusi kina cha maji , kimsingi Diamond ana supporter kubwa Sana ndani na nje ya nchi, si kama mshindani wake Burnaboy Ila kuliko msanii yyte Kwa ukanda wa Africa mashariki na pengine na Kati.


Hvyo kundi hili wanaona wakimpa support Burnaboy na yeye Kwa namna moja ama nyingine akitambua hlo basi atakuwa tayar kuwa karbu na Harmonize na Harmonize atamtumia kama ngazi ya kumpaisha ili lengo Lao lifanikiwe .....


Diamond anajua kutumia fursa , kitendo cha yeye kuwa nominated , na stuation inayoendelea Mitandaoni inampa mileage kubwa Sana kuwafikia wasaniii wa kiwango cha juu zaidi duniani ....


Vyovyote itakavyokuwa kufanikiwa Kwa lengo Lao kutategemea , bahati na nyota ya msanii wao....na sio kelele za kutaka fulan ashindwe ili fulani apae ....nafkri hzo sarakasi Diamond amecheza nazo tangu anatoka sharobaro record mpak hvi leo ...

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger