Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Hawa Nao Watupumzishe...Beka Afunguka Kumwagana Tena Na Mkewe

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
MSANII anayefanya poa kunako gemu la Bongo Fleva, Bakari Katuti ‘Beka Flavour’ amefunguka juu ya tetesi zinazosambaa kuwa amemwagana tena na mkewe anayejulikana kwa jina la Happyness.


Kupitia Gazeti la IJUMAA, staa huyo anasema kuwa, katika maisha yake hajawahi kuoa na anachokijua yeye Happy ni mzazi mwenzake na wala siyo mke wake, hivyo haoni sababu ya kumuongelea, lakini ambacho watu wanatakiwa wakifahamu kwa sasa kuhusu yeye ni kwamba yupo singo.


“Mimi sijawahi kuoa na wala sina mpango wa kuoa leo wala kesho.


Kwa hiyo sina mke ila ninachokijua ni kwamba nina mwenzangu ambaye kwa sasa tumebaki kulea tu mtoto wetu, hivyo jimbo liko wazi, kwa ufupi nipo singo,” anasema Beka anakimbiza Ngoma ya Bahati Mbaya.

Stori: IMELDA MTEMA, DAR

Post a Comment

0 Comments