Kisa Manyama, Simba Waifuata Azam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




TAARIFA za chini ya kapeti zinaeleza kuwa, Uongozi wa Klabu ya Simba umeufuata uongozi wa kikosi cha klabu ya Azam kwa ajili ya kuomba kuachiwa nafasi ya kumsajili aliyekuwa beki wa Ruvu Shooting, Edward Charles Manyama.

 

Azam tayari wamemtangaza Manyama kuwa mchezaji wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu, huku wakati huohuo Simba walikuwa wakitajwa kumalizana na nyota huyo.

 

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikosi cha Azam kimelitonya Championi Jumatatu, kuwa Simba wameufuata uongozi wa Azam kuomba kuachiwa mchezaji huyo.

 

“Unajua ishu ya Manyama kuhitajika na Simba ni jambo lililo na uzito mkubwa sana kiasi kwamba, kuna baadhi ya viongozi wao wamekuja kujaribu kuongea na viongozi wetu ili tuwaachie, lakini tayari uongozi wetu uliwaambia tuna mipango naye.

 

”Alipotafutwa Ofisa habari wa Klabu ya Azam, Zakaria Thabit, Zaka Zakazi kuzungumzia suala hilo alisema: “Watu wengi hawajui kuwa sisi Manyama tulimalizana naye mapema, kabla ya hizo tetesi za klabu ya Simba kumhitaji, hivyo ninachojua mimi Manyama ni mchezaji wetu na si vinginevyo.”

STORI: JOEL THOMAS, Dar es Salaam


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad