.

6/02/2021

Kunilinganisha na Messi, Ronaldo ni kujitoa ufahamu – Kylian MbappeMchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na Klabu ya PSG, Kylian Mbappe amesema kuwa hawezi kulingana hata chembe na wachezaji bora kabisa duniani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo huku akisisitiza kuwa kumlinganisha yeye na nyota hao ni kujitoa ufahamu kutokana na makubwa waliyofanya kwa muda mrefu kwenye mchezo wa soka.Mshambuliaji huyo wa PSG, Mbappe amekuwa pia akitajwa yeye na nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haaland kama ‘Copy’ ya Messi na Ronaldo na hivyo Dunia ikiwatarajia mambo makubwa mnoo kutoka kwao baada ya ufalme wa mchezaji wa Juventus na Barca utakapofikia mwisho.

Akiwa kwenye umri wa miaka 22, tayari Mbappe ameshanyakuwa taji la kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Ufaransa mwaka 2018, mataji manne (4) ya Ligue 1 , mataji matatu (3) ya French Cups na mawili (2) ya French League Cups, lakini pia akifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya Champions League akiwa na PSG.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger